Search citation statements
Paper Sections
Citation Types
Year Published
Publication Types
Relationship
Authors
Journals
Msingi wa makala haya ni “Sera ya Elimu na Mafunzo” (SEM, 2014). Makala yanahakiki nafasi ya lugha ya Kiswahili kwenye Sera ya Elimu na Mafunzo nchini Tanzania na mustakabali wake kwenye mfumo wa elimu kama lugha ya kufundishia. Mbinu iliyotumika ni ya maktabani ambapo mwandishi alisoma na kuhakiki maudhui ya SEM msisitizo ukiwa kwenye masuala yahusuyo lugha ya kufundishia. Uchambuzi wa kiisimujamii ulitumika ili kuonesha ukinzani baina ya matamko ya SEM. Tamko la SEM kuhusu lugha ya Kiswahili kama lugha ya kufundishia haliakisi hali halisi. Uhusiano wa Kiisimujamii wa lugha ya Kiswahili na ya Kiingereza kuhusu elimu unatoa tafsiri kuwa endapo SEM itatumika bila nia ya dhati ya kuisaidia lugha ya Kiswahili basi lugha hiyo inaweza kutoweka kabisa kwenye mfumo wa elimu kama lugha ya kufundishia. Makala yanajenga hoja kuwa tamko la SEM kwamba Kiingereza na Kiswahili ziwe na hadhi sawa kwenye mfumo wa elimu linatia moyo kwa mustakabali wa lugha ya Kiswahili lakini utekelezaji wake unaibua changamoto nyingi kwa namna ambayo zisipotazamwa kwa makini lugha ya Kiingereza itaendelea kukita mizizi zaidi na kujenga uwezekano wa jamii kukataa kufundishwa kwa lugha ya Kiswahili kwa sababu mwelekeo wa jamii unanasibisha elimu na Kiingereza. Mwisho, wito unatolewa kwa watunga sera kusitisha kutumia lugha ya wachache kutoa elimu kwa wengi kwa kuwa kufanya hivyo ni kubadili malengo ya elimu.

Makala hii inahusu Kiswahili katika taathira ya kihistoria na mielekeo ya kisiasa kama lugha ya kufundishia elimu ya juu hapa nchini Tanzania. Makala hii inaeleza mambo yanayosababisha mielekeo tofauti ya watu kuhusu upokezi na matumizi ya lugha ya Kiswahili kama lugha ya kufundishia elimu ya juu nchini Tanzania ili kushurutishaukubalifu wake. Baadhi ya masuala yanayochunguzwa ni yale yanayotiliwa shaka kuhusu uwezo wa lugha ya Kiswahili kumudu na kukidhi harakati za mahitaji ya kufundishia elimu ya juu, pamoja na kupitisha teknolojia mpya inayoinukia katika nyanja za sayansi nateknolojia. Aidha, makala hii inanuia kufafanua ukubalifu, pamoja na msingi wa mielekeo ya Watanzania kutoipatiakipaumbele lugha ya Kiswahili kama lugha inayoweza kukidhi mahitaji ya kufundishia elimu ya juu hapa nchini. Data za msingi katika makala hii zilipatikana maktabani kwa kudurusu nyaraka mbalimbali zilizohusiana na mada iliyolengwa. Mapitio ya nyaraka mbalimbali zilizotumika kushadidia data za msingi za mada iliyochunguzwa zilipatikana katika maktaba ya chuo kikuu cha Kikatoliki cha Ruaha iliyopoIringa. Makala hii inahitimisha kwamba lugha za kigeni na zile za kiasili zinaweza kuendelea kutumika pamoja katika ngazi zote za elimu ili kuziwezesha kutekeleza vema dhima zake.
scite is a Brooklyn-based organization that helps researchers better discover and understand research articles through Smart Citations–citations that display the context of the citation and describe whether the article provides supporting or contrasting evidence. scite is used by students and researchers from around the world and is funded in part by the National Science Foundation and the National Institute on Drug Abuse of the National Institutes of Health.
customersupport@researchsolutions.com
10624 S. Eastern Ave., Ste. A-614
Henderson, NV 89052, USA
This site is protected by reCAPTCHA and the Google Privacy Policy and Terms of Service apply.
Copyright © 2025 scite LLC. All rights reserved.
Made with 💙 for researchers
Part of the Research Solutions Family.