Suala la ardhi limekuwa nyeti tangu jadi. Wahusika hutumiwa na wasanii kubainisha suala hili. Tafiti za awali zilijikita katika motifu ya safari, siri na maisha ya dunia. Hata hivyo, hakuna utafiti umefanywa kutathmini ujenzi wa motifu ya mgogoro wa ardhi kupitia wahusika. Makala hii imelenga kuziba pengo hili. Utafiti huu ni kutathmini ujenzi wa motifu ya suala la mgogoro wa ardhi kupitia wahusika; mfano kutoka Chozi la Heri na Kovu Moyoni. Motifu hii ni kurudiwarudiwa kwa suala la mgogoro wa ardhi baina ya wahusika katika matini teule. Makala hii iliongozwa na nadharia mbili; Nadharia ya Uhalisia wa Kijamaa na Nadharia ya Sosholojia ya Fasihi. Nadharia ya Uhalisia wa Kijamaa iliwaongoza watafiti kuweza kubainisha suala la ardhi kama lilivyoangaziwa na waandishi katika uhalisia wake. Hata hivyo, nadharia hii ilipungukiwa kubainisha jinsi matabaka katika jamii huendeleza suala la ardhi. Nadharia iliyofidia pengo hili ni Sosholojia ya Fasihi. Utafiti huu ulikuwa wa maktabani ambapo matini teule ziliteuliwa kimaksudi. Mpango wa kimaelezo ulitumika kuchanganua na kuwasilisha matokeo. Matokeo ya makala hii ni kuwa motifu ya mgogoro wa ardhi imekuzwa kupitia kwa wahusika antagonisti, protagonisti, tuli na bui. Kwa hivyo, utachangia katika uhakiki wa kazi za baadaye za nathari za fasihi ya Kiswahili. Aidha, walimu na wanafunzi wataelewa namna wahusika hujengwa. Makala hii ilipendekeza tafiti za baadaye zifanywe kutathmini motifu ya wahusika katika sekta ya uchumi na siasa.
Sanaa za kihalisia-ajabu husheheni usimulizi wa matukio yasiyotafsirika wala kufikirika kuwa na uyakinifu katika maisha ya mwanadamu. Fasihi za aina hii hutilia nguvu umazingaombwe na kukiuka uhalisia. Riwaya ya Babu Alipofufuka ya Mohamed ni mfano mojawapo wa fasihi yenye uhalisia-mazingaombwe. Utafiti huu unapambanua mkabala huo kwa kusimikwa kwenye mada Mustakabali wa Uongozi katika bara la Afrika katika karne ya 21: Tathmini ya Uhalisia-ajabu katika Riwaya ya Babu Alipofufuka na Said Ahmed Mohamed. Malengo ya utafiti huu ni; Kupambanua uhalisia-ajabu na uozo wa uongozi na hatimaye kutambua suluhu kwa matatizo ya uongozi barani Afrika kwa mujibu wa riwaya ya Babu Alipofufuka. Uchunguzi katika kazi hii uliongozwa na nadharia ya uhalisia-ajabu kwa kujifunga kwa mihimili yake mitano: kinaya, uandishi ndani ya uandishi, umazingaombwe katika mukhtadha halisi, vurugu la kiwakati na muingilano wa matini. Utafiti wenyewe uliendeshwa kwa mtindo wa kimakusudi ambapo matini maalum zilichanganuliwa maktabani na vile vile mtandaoni. Mbinu ya uchanganuzi ilihusu yaliyomo katika riwaya ya Babu Alipofufuka. Mhakiki pia alilenga kuchanganua kazi nyingine za fasihi kwa misingi ya malengo ya utafiti huu. Matokeo ya uchunguzi huu yana umuhimu mkubwa kwani yatasaidia kuchunguza suala la uongozi katika kutatua matatizo ya ndani kwa ndani kwa mustakabali wa itikadi za Kiafrika. Uchunguzi huu unashikilia kuwa utandawazi ni nduli ambalo limechangia kuwepo kwa matatizo humu barani na kuzidi kuifanya Afrika kunyongeka katika minyororo ya utumwa mpya. Taswira hii ni dhahiri katika riwaya mpya za Kiswahili. Matokeo yake bila shaka yatapevua ufahamu kuwa Afrika ina itikadi za kijadi ambazo zilizingatiwa katika kutafuta suluhu kwa matatizo ya ndani kwa ndani hasa za kisiasa. Wanafunzi wa shule za upili na vyuo vikuu pia watanufaika na matokeo ya uchunguzi huu kwa kupata mwelekeo wa uhakiki wa kazi za fasihi mintarafu zenye uhalisia-ajabu.
scite is a Brooklyn-based organization that helps researchers better discover and understand research articles through Smart Citations–citations that display the context of the citation and describe whether the article provides supporting or contrasting evidence. scite is used by students and researchers from around the world and is funded in part by the National Science Foundation and the National Institute on Drug Abuse of the National Institutes of Health.
customersupport@researchsolutions.com
10624 S. Eastern Ave., Ste. A-614
Henderson, NV 89052, USA
This site is protected by reCAPTCHA and the Google Privacy Policy and Terms of Service apply.
Copyright © 2025 scite LLC. All rights reserved.
Made with 💙 for researchers
Part of the Research Solutions Family.