Katika makala haya, watafiti anaeleza jinsi usimulizi wa hadithi umeathiriwa na usasa katika jamii ya Wamasaaba nchini Uganda. Anafanya hivyo kwa kulinganisha hali ilivyo sasa na jinsi ilivyokuwa kabla Wazungu hawajazuru barani Afrika. Mtafiti analinganisha miktadha ya utendaji wa hadithi na anatoa maelezo kuhusu mitindo mbalimbali ya utendaji. Anaeleza jinsi Waafrika walivyosimulia watoto wao hadithi kabla ya Wazungu kuja barani humu. Kwenye kazi hii, madhumuni ya utafiti ni: kudhihirisha athari za usasa kwenye masimulizi ya kinathari. Pili, kueleza stadi zilizokuwa zikitumiwa na Waafrika katika usimulizi wa hadithi. Mkabala wa utafiti ulikuwa wa nyanjani. Kwa kutumia mkabala huu, mtafiti alizuru nyanjani halafu akaanza kuendeleza mahojiano na wahojiwa wake. Kabla hajafanya hivyo, mtafiti alijitambulisha kwa wahojiwa wake na kuwaambia sababu za utafiti wake. Alifanya hivyo ili kuwaondolea wasiwasi. Majibu ya wahojiwa yalijumlisha data ambazo zilihitajika na mtafiti. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa usimulizi wa hadithi umefifia sana katika jamii ya Wamasaaba kutokana na usasa. Sababu ambazo zimepelekea usimulizi wa hadithi kufifia jamii hii pia zimeelezwa. Miongoni mwa sababu hizo ni: ulevi ambao hufanya watu kurejea nyumbani wakiwa wamelewa na kushindwa kusimulia watoto wao hadithi. Sababu nyingine ni wazazi kuthamini elimu ya kisasa na kuacha utamaduni wao wa kulea watoto ili baadaye wawe wake na waume wazuri. Wazazi kuhamasisha watoto wao wasome vitabu badala ya kuwasimulia hadithi. Nne, wazazi kuwa na lengo la kuelimisha watoto wao ili baadaye wapate kazi za afisi. Tano, jambo la kuwepo na utandawazi ambalo limepelekea watu kujumuika na kuiga tamaduni za kigeni. Upeo wa utafiti huu ulihusika na mabadiliko kwenye usimulizi wa hadithi na sababu ambazo zimepelekea utamaduni wa kusimulia hadithi kufifia katika jamii ya Wamasaaba nchini Uganda. Mtafiti alitumia mbinu ya bahati nasibu kuteua sampuli za wahojiwa.
Katika makala haya, mtafiti anaeleza jinsi lugha inavyotumiwa na wazazi katika shughuli ya kuelekeza mabinti zao katika maisha ya ndoa. Anafanya hivyo kwa kurejelea ndoa za kijadi katika jamii ya Wamasaaba nchini Uganda. Kwa kurejelea jamii hii, mtafiti anaeleza namna wazazi wanavyotumia lugha kuelekeza mabinti zao katika mambo yanayopelekea ndoa zao kudumu. Mtafiti alinukuu baadhi ya semi ambazo zinasemekana kuwa zinatumiwa na wazazi katika shughuli hiyo. Ni kweli kwamba lugha yoyote ile huwa inafanya kazi nyingi sana kama vile kutumbuiza watu, kutongozana, kugombana, kufundisha, kuelekeza, n.k. Hii ni kwa sababu bila kutumia lugha, mtu hawezi akaimba wimbo, akagombana, akafundisha, na akaelekeza. Hata hivyo, katika makala hii, mtafiti anajikita kwenye mchango wa lugha katika maisha ya ndoa. Katika kazi hii, mtafiti anazingatia semi mbalimbali ambazo Wamasaaba huzitumia kwa ajili ya kuelekeza mabinti zao katika masuala ya ndoa. Katika jamii mbalimbali, watu hutumia lugha kutekeleza jambo hili. Jamii hasa zile za jadi zilitumia lugha kuelekeza mabinti katika mambo ya ndoa. Kuna namna ambavyo walisuka lugha kisanaa kwa lengo la kufunza mabinti maisha ya ndoa. Hii ni kwa sababu hawakuwa na madarasa maalumu mwa kufunzia watoto wao kama ilivyo sasa. Katika jamii hizo, shule zenyewe hazikuwepo. Kwa hiyo, lugha ndiyo ilikuwa chombo maalumu cha kufunzia watoto. Matumizi ya lugha yalidhamiria kukuza mabinti ambao wangevumilia maisha ya ndoa. Hivyo basi, katika kazi hii, mtafiti anajikita katika matumizi ya lugha na kueleza jinsi Wamasaaba wanavyotumia semi mbalimbali kuelekeza mabinti zao katika masuala ya ndoa.
Katika makala hii, mwandishi anaeleza maudhui mbalimbali yanayopatikana katika nyimbo za tohara za Wamasaaba nchini Uganda. Alifanya hivyo kwa kurejelea angalau mfano mmoja wa nyimbo hizo kwa kila maudhui. Mwandishi amepanga maudhui hayo kulingana na utaratibu wa utendaji wa matukio ya tohara. Kutokana na jambo hili, mwandishi ameangalia matukio mbalimbali katika utekelezaji wa tohara kwa sababu nyimbo hizo huambatana na matukio fulani. Kwa kufanya hivyo, mwandishi ametaja tukio na kutoa mfano wa wimbo unaoimbwa. Baada ya kutoa mfano wa wimbo, anauchanganua na kubainisha maudhui mbalimbali yaliyomo. Mwandishi anafanya hivyo hatua kwa hatua mpaka mwisho. Dhamira ya utafiti ni kueleza jinsi Wamasaaba walivyobobea katika utanzu huu wa sanaa. Hali kadhalika, madhumuni ya utafiti huu ni kueleza namna nyimbo za kiutamaduni zilivyo muhimu katika maisha ya binadamu, kufafanua athari za nyimbo za tohara kisaikolojia na kuonyesha nguvu za mawasiliano za nyimbo za kiutamaduni. Mkabala wa utafiti huu ulikuwa wa nyanjani. Kwa kutumia mkabala huu, mtafiti alizuru nyanjani na kukusanya nyimbo. Katika kazi yake, mtafiti alitumia mbinu ya uchunguzi shiriki. Kwa kutumia mbinu hii, mtafiti alifuatilia makundi ya watendaji na kushuhudia jinsi matukio ya tohara yanavyotekelezwa. Kulingana na aina ya utafiti, mtafiti hakuuliza watu maswali. Mtafiti alitumia kinasa sauti kurekodi nyimbo. Baada ya mchakato huo kukamilika, mtafiti alizichanganua nyimbo ambazo alizikusanya halafu akawasilisha matokeo ya utafiti wake. Nyimbo zilizokusanywa zilijumlisha zile za kupokea wageni, zile zinazoonyesha huzuni kwa mhusika, zile zinazodhihirisha furaha kwa mhusika, zile za kuonya mhusika nk. Mtafiti alianza uchanganuzi wa nyimbo kwa kuziandika kwenye karatasi. Baada ya kufanya hivyo, alizipanga kulingana na madhumuni ya utafiti. Alipomaliza kufanya hivyo, mtafiti alieleza maudhui mbalimbali kama yalivyojitokeza katika kila wimbo.
In this paper, the authors explain how language usage can affect human resource performance. They do that by explaining how language can be used in different institutions. Authors provide their explanations by referring to Bududa Local district government. The study's objectives were to explain the importance of human resources in organisations and the usefulness of language usage in human resource performance. The research problem is that in Uganda, language usage has not been emphasised so much as a key element in human resource performance. In this study, the researchers used a case study and field research designs. By using this particular research design, they interviewed only a few people and the results were used to represent the whole District. The researchers used the staff in different departments as their respondents following their experience. The researchers tallied the data and gave the frequency of each role of language usage in human resource performance. After tallying the data, the results were presented by the use of tables. The study's findings are as follows: promoting unity among the employees, promoting love among the employees, giving employees the zeal to do the work, making the employees develop the spirit of belonging, and developing a collective responsibility spirit.
Katika makala hii, mtafiti anaeleza jinsi vitenzi vya lugha za Kiafrika vinavyonyambuliwa na kuleta maana tofauti tofauti. Anafanya hivyo kwa kurejelea Kimasaaba ambayo ni lugha inayozungumzwa na Wamasaaba nchini Uganda. Unyambuaji wa vitenzi ni jambo la kawaida na huwa linatekelezwa katika lugha mbalimbali. Hivyo basi, katika makala hii, mtafiti anaeleza mnyambuliko ya vitenzi katika lugha ya Kimasaaba. Anawasilisha mkusanyiko wa vitenzi na kueleza jinsi vinavyonyambuliwa na wazungumzaji. Aidha, mtafiti anaeleza namna vitenzi hivyo vinatumiwa katika sentensi. Mtafiti anafanya hivi kwa sababu lugha nyingi za Kiafrika hazijatafitiwa na kuna mambo mengi sana mazuri ambayo hayajulikani kwa ulimwengu. Katika kazi hii, mtafiti anaandika vitenzi mbalimbali katika lugha asili halafu anavitafsiri katika Kiswahili. Kwenye kazi hii, madhumuni ya utafiti ni kudhihirisha utaratibu wa kunyambua vitenzi katika Kimasaaba. Pili, kueleza maana tofauti zinazotokana na mnyambuliko ya vitenzi. Tatu, kuonyesha kuwa Kimasaaba ni lugha inayoendelea kukua kama lugha zingine za Kiafrika. Mkabala wa utafiti ulikuwa wa nyanjani. Kwa kutumia mkabala huu, mtafiti alizuru nyanjani ambako aliendeleza mahojiano na wahojiwa wake. Majibu ya wahojiwa yalijumlisha data ambazo zilihitajika na mtafiti. Mwishowe, matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwa Kimasaaba kama lugha nyingine za Kiafrika ina vitenzi vingi sana vinavyonyambuliwa na kwendeleza mazungumzo ya wazungumzaji.
scite is a Brooklyn-based organization that helps researchers better discover and understand research articles through Smart Citations–citations that display the context of the citation and describe whether the article provides supporting or contrasting evidence. scite is used by students and researchers from around the world and is funded in part by the National Science Foundation and the National Institute on Drug Abuse of the National Institutes of Health.
customersupport@researchsolutions.com
10624 S. Eastern Ave., Ste. A-614
Henderson, NV 89052, USA
This site is protected by reCAPTCHA and the Google Privacy Policy and Terms of Service apply.
Copyright © 2025 scite LLC. All rights reserved.
Made with 💙 for researchers
Part of the Research Solutions Family.